Tumedhamiria kushinda kila taji - Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
20 Aug 2018
Tumedhamiria kushinda kila taji - Kichuya
Baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Mtibwa Sugar, kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, ametamba kuwa huo ni mwanzo, hivyo wamepanga kutwaa mataji yote ya makombe watakayoshiriki msimu huu.

Simba imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuwafunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere na Hassani Dilunga huku lile la Mtibwa Sugar likifungwa na Kelvin Sabato.

Kichuya amesema kuwa hakuna kitakachoshindikana kwao kutokana na ubora wa kikosi chao na morali iliyopo kwa wachezaji.

Kichuya ameongeza kuwa Ngao ya Jamii waliyoipata itakuwa mwanzo mzuri kwao katika kuelekea msimu mpya wa ligi, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Jumatano.

“Nianze kwa kuwashukuru mashabiki wa Simba kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutupa sapoti ambayo imetuongezea morali ya sisi kupambana na kupata matokeo hayo mazuri," Kichuya ameliambia gazeti la Championi

“Kikubwa mashabiki wetu wasiache kujitokeza uwanjani kwa ajili ya kutupa sapoti na tunawaambia hatutawaangusha tukielekea katika msimu mpya wa ligi ambao hatuachi kitu, tumepanga kuchukua makombe.

“Tumeanza na Ngao ya Jamii, hivi sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye ligi huku tukijiandaa na mashindano mengine yanayokuja,” alisema Kichuya.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →