Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Kaimu Rais wake, Salim Abdallah 'Try Again' umesema kikosi walichonacho hivi sasa kitazidi kuwa bora zaidi ya wapinzani wao.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii kumalizika jijini Mwanza jana, Abdallah alisema kwa namna kikosi ambacho wanacho kitazidi kuonesha matunda kwenye msimu ujao wa ligi.
Kiongozi huyo amefunguka akiamini kitendo cha kuchukua Ngao hiyo mbele ya Mtibwa kimewafungulia njia nzuri ya kuanza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao.
"Kwa kikosi hiki tulichonacho kitakuwa bora zaidi na hii ni kutokana na namna uongozi ulivyopambana kusajili wachezaji ambao watakipigania kupata matokeo, ni mwanzo mzuri kuelekea ligi ya msimu ujao" alisema.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kupitia kwa straika hatari Meddie Kagere na Hassan Dilunga na kuipa timu taji hilo la kwanza ikiwa na Kocha wake mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems.

ADVERTISE HERE