Baada ya hapo jana kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 na kutwaa Ngao ya Jamii, kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea leo jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Prisons.
Mchezo huo utapigwa Jumatano, August 22 siku ya Iddi kwenye uwanja wa Uhuru.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba Haji Manara amesema wachezaji wamepata mzuka zaidi baada ya kutwaa Ngao ya Jamii na sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye michezo ya ligi.
Kikosi cha Prisons kinatarajiwa kutua jijini Dar es salaam kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao umehamishiwa uwanja wa Uhuru baada ya uwanja wa Taifa ambao utakuwa na matumizi mengine.

ADVERTISE HERE