FT : Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Ngao ya Jamii yarudi Msimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Aug 2018
FT : Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Ngao ya Jamii yarudi Msimbazi
Simba imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba Jumamosi jioni.



Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na nusura Emanuel Okwi afunge bao mapema tu kwenye dakika ya tatu baada ya shuti lake alilopia nje ya 18 kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.

Baada ya kosakosa nyingi, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika ya 29 akimalizia pasi murua ya kiungo aliyen'gara kwenye mchezo huo Hassani Dilunga.



Mtibwa Sugar ilisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 33 kupitia kwa Kelvin Sabato aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18.

Dilunga akaifungia Simba bao la pili kwenye dakika za majeruhi kipindi cha kwanza kwa shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Mtibwa Benedictor Tinocco.



Dilunga aliyesajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar hakushangilia bao hilo,aliomba radhi likiwa ni tukio la kiungwana kuwafanyia waajiri wake hao wa zamani.

Licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu kwenye kipindi cha pili, ni Simba iliyofanikiwa kulinda ushindi wake na kutwaa Ngao hiyo ya jamii.



Aidha katika kipindi hicho Simba ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Emanuel Okwi kuumia huku nafasi yake kuchukuliwa na nahodha John Bocco.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’