Simba vs Mtibwa Sugar, kitaeleweka CCM Kirumba leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Aug 2018
Simba vs Mtibwa Sugar, kitaeleweka CCM Kirumba leo
Baada ya majigambo na maandalizi ya muda mrefu, hatimaye mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wanatarajia kuwavaa wababe wa Kombe la FA, Mtibwa Sugar katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii itakayofanyika leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Simba inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mechi ya kuwania ngao hiyo mwaka jana baada ya kuwafunga Yanga penalti 5-4.

Akizungumzia mchezo huo wa leo, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika na kazi imebaki kwa wachezaji wake.

"Kila kitu kipo sawa, kama walimu kazi tumeimaliza na imebaki kazi ya wachezaji uwanjani, hatutegemei mchezo kuwa mwepesi, lakini tutapambana kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Djuma.

Alisema mapungufu yaliyobainika katika mechi za kirafiki yamefanyiwa kazi na sasa wanawataka wachezaji kuonyesha matunda ya maandalizi waliyoyafanya wakiwa nje na ndani ya nchi.

"Siwezi kusema kwa sasa ni mbinu gani tutatumia, lakini kama umeona michezo yetu ya kirafiki tuliyocheza unaweza ukajua nini tutafanya, kikubwa tunataka ushindi na hatutarajii kuwaangusha mashabiki wetu," alisema Djuma.

Kikosi hicho cha Simba kitamkosa kiungo wake anayekuja juu Mzambia, Clatous Chama ambaye bado hajapata hati ya uhamisho ya kimataifa (ITC).

Pia Simba huenda ikawakosa nahodha John Bocco na beki Shomari Kapombe ambao wamepona majeraha yao hivi karibuni

Naye Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alisema kuwa kikosi chake hakina hofu yoyote ya kuwakabili Simba kwa sababu walifanya maandalizi mazuri.

"Simba ni timu nzuri na wamefanya maandalizi mazuri, ila nakiamini kikosi changu na nimewaangalia Simba kwenye michezo yao ya kirafiki, kuna kitu cha kiufundi nimekipata," alisema Katwila.

Simba wanacheza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa mara ya sita tangu kuanzishwa kwake huku wapinzani wao, Mtibwa Sugar wakicheza kwa mara ya pili na mechi hiyo ya leo ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza Agosti 22 mwaka huu.

IPP Media
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’