Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' leo amekutana na kufanya mazungumzo na kocha wa viungo wa timu hiyo Adel Zrane kutoka nchini Tunisia.
MO amesema kocha huyo ana majukumu muhimu katika kikosi cha Simba kuhakikisha wachezaji wote wanakuwa 'fiti' msimu mzima.
"Nimekutana na kocha wetu wa viungo Adel Zrane kutoka Tunisia. Ana moja ya majukumu muhimu katika Simba - kuwafanya wachezaji wetu kuwa fiti kucheza na imara wakati wote wa msimu," amesema MO.
Kikosi cha Simba kiko jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa keshokutwa Jumamosi, August 18 kwenye dimba la CCM Kirumba mkoani Mwanza.

ADVERTISE HERE