Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba wametimiza ahadi ya kuondoka na ushindi mkoani Arusha baada kuilaza Arusha United mabao 2-1.
Mabao yote ya mchezo huo yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza Emanuel Okwi akifunga mabao ya Simba huku bao pekee la Arusha United likifungwa na Ally Kabunda.
Idadi kubwa ya mashabiki kutoka kila kona ya mkoa wa Arusha walifurika kwa wingi uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuushuhudia mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda.
Simba inatarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Mwanza tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumamosi, August 18 kwenye uwanja wa Taifa.

ADVERTISE HERE