Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema ataachia ngazi ndani ya klabu hiyo endapo timu yake itapoteza mchezo dhidi ya Arusha United leo.
Manara ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa leo wa kirafiki kati ya Arusha United dhidi ya Simba
Mchezo huo uliovuta hisia za wakazi wa mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani utatumika kuiandaa Simba kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa August 18 mkoani Mwanza.
Ofisa huyo amefunguka akiamini kuwa Simba haiwezi kufungwa na Arusha United huku akitamba kumuahidi kipigo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye ndiye mlezi wa Arusha United.
"Kama Arusha United wakishinda leo mimi nitaachia rasmi ngazi ndani ya Simba, siamini kama wanaweza wakatufunga" alisema.
Mgeni rasmi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda aliyepewa mwaliko rasmi na Mh Gambo.

ADVERTISE HERE