Simba yaipigia 'tizi' Mtibwa Sugar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Aug 2018
Simba yaipigia 'tizi' Mtibwa Sugar
Kikosi kamili cha Simba kitakachoanza katika mechi ya Ngao ya Jamii itayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Agosti 18 dhidi ya Mtibwa Sugar kimewekwa wazi.

Kikosi hicho kimefichuka katika mazoezi ya Simba ya leo Jumatatu walifanya asubuhi uwanja wa Gymkhana na baada ya kumaliza nyota wote walikwenda kambini Sea Scape kabla ya kuanza safari ya kwenda Arusha jioni yake.

Simba watacheza mechi ya kirafiki na Arusha United ambayo inanolewa na kocha Fred Felix Minziro kabla ya kuondoka na pipa kwenda Mwanza kuwakabili Mtibwa ambao nao waliweka kambi hapa Dar es Salaam.

Kulingana na mazoezi ya Simba ambayo pia walifanya uwanja wa Uhuru kocha wa Simba, Patrick Aussems amekuwa akiwapa nafasi ya kucheza katika kikosi kimoja baadhi ya nyota ambao huenda ndio kikawa kikosi cha kwanza.

Nyota waliokuwa ni kipa Aishi Manula, mabeki Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Pascal Wawa ambaye amekuwa akipokezana na Yusuph Mlipili sambamba na Erasto Nyoni.

Katika viungo wapo James Kotei ambaye amekuwa akipishana na Hassan Dilunga pamoja na Jonas Mkude.

Mawinga kushoto alikuwa akicheza Shiza Kichuya, kulia Cletus Chama wakati washambuliaji wa kati ni Meddie Kagere alikuwa akipishana na Adam Salamba huku Emmanuel Okwi akicheza na muda mwingine kabla ya mazoezi kumalizika anapishana na Mohammed Rashid.

Simba mpaka wanachukua ubingwa chini ya Mfaransa Pierre Lechantre na msaidizi wake Masoud Djuma walikuwa wakicheza mfumo wa (3-5-2) lakini tangu ujio wa Aussems ametengua mfumo huo na sasa wanatumia (4-4-2).

"Haya mazoezi na mechi za kirafiki ambazo tunacheza mchezaji yoyote anaweza kupata nafasi kikosi changu kwani wote wapo vizuri na naamini katika viwango vyao.

"Tumetoka katika mazoezi magumu nchini Uturuki ninachoangalia sasa ni kupata kikosi na ndio maana nimekuwa nikitoa nafasi kwa kila mchezaji ili kuona yupi anafaa kumtumia kulingana na mechi husika," alisema Aussems.

Meneja wa Simba, Richard Robert alisema "Nadhani hiyo Simba ambayo ilikuwa inacheza katika mechi za kirafiki tulikuwa tupo kwenye majaribio baada ya kutoka katika mazoezi magumu lakini kikosi kamili mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona Simba kamili dhidi ya Mtibwa".

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’