Mahakama yatoa siku saba, HansPoppe na Lauwo waondolewe kesi ya Aveva

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Aug 2018
Mahakama yatoa siku saba, HansPoppe na Lauwo waondolewe kesi ya Aveva
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa wawili katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu au kuifuta kesi hiyo.

Washtakiwa wanaotakiwa kuondolewa katika kesi hiyo ni Zacharia Hanspope na Frank Lauwo ambao hawajawahi kufika mahakamani hapo.

Akitoa uamuzi huo leo mahakamani hapo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema bado wanaifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu lakini itafika mahali uvumilivu utawashinda na kama jamhuri wameshindwa basi waifute. β€œUkiangalia afya ya Aveva unaona kabisa ni mgonjwa, anatakiwa kwenda kliniki kwa wiki mara mbili, hivyo basi tunalazimika kuangalia ratiba ya matibabu yake ili tupange kesi,” amesema Hakimu Simba.

Awali, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na tayari wameshaifanyia marekebisho hati ya mashtaka na kwamba wanasubiri kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kesi hiyo iendelee kwa mujibu wa sheria.

Baada ya Wakili huyo kudai hayo, Aveva aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibu za kusikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa imechukua muda mrefu huku Wakili wa Jamhuri Shadrack Kimaro na Wakili Takukuru, wamekuwa wakirushiana mpira.

Kwa upande wake Kaburu ambaye ni mshtakiwa wa pili amedai kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita wako mahabusu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo huku mawakili hao wakidai faili liko kwa DPP.

Alidai mshtakiwa wa kwanza, Aveva ana matatizo ya kiafya na kwamba kila wiki anaenda kliniki kwa ajili ya matibabu hivyo basi kuendelea kurushiana mpira ni kuwaumiza na kwamba hadhani kama DPP ameshindwa kushughulikia kesi yao, bali ni ucheweshaji wa makusudi unaofanywa na mawakili hao katika kesi hiyo kutoka kwa DPP na Takukuru.

Amedai upelelezi umeshakamilika kilichobaki ni kubadilisha hati hiyo ili kesi ianze kusikilizwa.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’