Aussems amtetea Salamba, asema kukosa penati sio ajabu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Aug 2018
Aussems amtetea Salamba, asema kukosa penati sio ajabu
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amemkingia kifua mshambuliaji wake, Adam Salamba baada ya kukosa penalti katika mechi ya juzi dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana na kusema kuwa si wa kwanza kukosa penalti.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, dakika chache kabla mpira kumalizika, Simba walipata penalti kupitia kwa Salamba aliyeangushwa ndani ya eneo la hatari, lakini mshambuliaji huyo alishindwa kufunga na kuipa timu yake goli la ushindi baada ya mpira kudakwa na kipa wa Asante Kotoko.

Akizungumza baada ya mchezo huo jzui, Aussems alisema ni jambo la kawaida kukosa penalti hivyo hawezi kumlaumu mchezaji huyo.

"Kukosa penalti kunatokea, hata wachezaji wakubwa wanakosa penalti..., Messi, Ronaldo huwa wanakosa kwa nini iwe ajabu kwa Salamba," alisema Aussems.

Aidha, Kocha huyo aliwasifia wachezaji wake wote kwa kujituma na kucheza vizuri licha ya matokeo ya sare waliyoyapata kwenye mchezo wao huo uliofanyika siku ya Tamasha la Simba Day.

"Tuna mchezo mwingine siku chache zijazo (Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa), tutatumia siku zilizobaki kujiandaa vyema..., sijaona mapungufu makubwa sana katika mchezo wa leo (juzi). Siku zilizobakia zitatosha kuweka mambo sawa," alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Simba inatarajia kuivaa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ngao ya Hisani itakayofanyika Agosti 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wakati huo huo kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka jijini leo na kuelekea Lindi kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Namungo FC itakayofanyika Jumamosi.

Mechi hiyo inachezwa sambamba na ufunguzi wa uwanja mpya uliojengwa na Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa.

IPP Media
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’