Nyoni, Mzamiru waondolewa kikosi cha Stars

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
4 Nov 2017
Nyoni, Mzamiru waondolewa kikosi cha Stars
Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amewaengua kwenye kikosi chake wachezaji wawili wa Simba, beki Etasto Nyoni na kiungo Muzamil Yassin kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin wiki ijayo.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema wachezaji hao wameenguliwa kutokana na kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Malawi Oktoba 7, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Lucas amesema katika utaratibu wake mpya, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linaagiza mchezaji anayeonyeshea kadi nyekundu hata katika mchezo usio wa mashindano, asitumike katika mchezo unaofuata.

“Sasa baada ya kupokea barua ya FIFA ikituzuia kuwatumia wachezaji hao katika mchezo ujao dhidi ya Benin, kocha amefanya mabadiliko hayo madogo,”amesema Lucas.

Lucas amesema kwamba baada ya kuenguliwa kwa Nyoni na Yassin, Mayanga amewaita viungo Mudathir Yahya kutoka Singida United na Jonas Mkude kutoka Simba SC.

Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu na kikosi cha wachezaji 24 kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.

Kikosi kamili cha Taifa Stars sasa ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afruka Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mudathir Yahya (Singida United), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Jonas Mkude (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Difaa), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya)

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →