Kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima hakuwa miongoni mwa wachezaji waliotambulishwa jana kwenye Tamasha la SIMBA DAY lililofanyika uwanja wa Taifa.
Niyonzima bado hajarejea nchini kuungana na mabingwa hao wa Tanzania Bara hivyo kuibua sintofahamu juu ya mustakabali wake.
Aidha usajili wa viungo Cletus Chama (fundi) na Hassani Dilunga unafanya hatma ya Niyonzima aliyesajiliwa kutoka klabu ya Yanga msimu uliopita kuwa mashakani.
Wakati Niyonzima hatma yake ikiwa haifahamiki, Mganda Juuko Murshid amerejea kwao Uganda na kusajiliwa na klabu ya Vipers FC.
Murshid amesajiliwa na Vipers siku chache zilizopita muda mfupi baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini alikokuwa akifanya majaribio katika klabu ya SuperSport.
hata hivyo licha ya taarifa hizo za Murshid kusajiliwa na Vipers, Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah amesema mchezaji huyo pamoja na Niyonzima bado ni wachezaji wa Simba.
Salim alisema kutoonekana kwao jana uwanjani hakumaanishi kuwa wao sio sehemu ya kikosi cha Simba kwa ajili ya msimu ujao.

ADVERTISE HERE