Simba kukitangaza kinywaji cha Mo Energy kwa Mil 250

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Aug 2018
Simba kukitangaza kinywaji cha Mo Energy kwa Mil 250
Klabu ya Simba imeingia mkataba wa Mwaka mmoja kukitangaza kinywaji cha Mo Energy. Mkataba huo una thamani ya mil 250.

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kusainiwa kwa mkataba huo baina ya Simba na A One Products, ambao ndio wazalishaji wa kinywaji hicho, Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah 'Try Again' amesema fedha hizo zimepelekwa katika kukamilisha zoezi la ujenzi wa uwanja wa Simba ulioko Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Aidha, Salim amesema mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji 'Mo' amekubali kuongeza fedha ili kuwezesha uwanja huo kukamilika haraka iwezekanavyo.

Klabu ya Simba pia imetangaza rasmi kuanzisha gazeti lake litakalofahamika kwa jina la SIMBA NGUVU MOJA.

Gazeti hilo litazinduliwa rasmi keshokutwa uwanja wa Taifa, siku ya kilele cha SIMBA DAY na litakuwa likitoka kila Jumamosi likiuzwa kwa Tsh 500 tu.

Pia kwenye mkutano huo uliofanyika Hotel ya Serena kulikuwa na uzinduzi rasmi wa jezi za Simba kwa ajili ya msimu ujao 2018/19 ambazo zitaanzwa kuuzwa kesho Jumanne saa kumi jioni jijini Dar es salaam na zitaanza kupatikana mikoani siku chache baadae.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’