Jana klabu ya Simba iliendesha zoezi la uchangiaji damu ambapo wanachama na mashabiki wa timu hiyo walijitokeza kwa wingi Karume, Ilala Boma Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi hilo.
Uongozi wa Simba umewashukuru wote waliojitokeza ambapo wachangiaji 200 wa mwanzo wamepata tiketi za VIP kutazama mechi ya Simva Vs Asante Kotoko, Agosti 8, 2018 katika kilele cha maadhimisho ya SIMBA, kwenye uwanja wa Taifa.
Baada ya zoezi hilo, klabu ya Simba ilifanya dua Maalum ya kuwaombea wote waliotangulia mbele ya haki, Makao Makuu ya Klabu hiyo Msimbazi, Jijini Dar es Salaam, ukiwa ni utaratibu uliowekwa na klabu hiyo kila mwaka.

ADVERTISE HERE