Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewaita mashabiki kufurika uwanja wa Taifa kushuhudia burudani kutoka kwa vijana wake watakapokuwa wakicheza na Asante Kotoko kutoka Ghana kwenye kilele cha tamasha la SIMBA DAY.
Simba ilitarajiwa kuwasili Alfajiri ya leo Jumatatu kutoka nchini Uturuki ilikokuwa imeweka kambi ya wiki mbili.
Aussems amesema anafahamu ukubwa wa siku hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu ya Simba. Siku ambayo mbali na mambo mengine, kikosi cha Simba cha msimu wa 2018/19 kitatambulishwa.
"Nafahamu siku hiyo inasubiriwa kwa hamu na kila Mwana Simba nchini Tanzania," amesema Aussems.
"Ni siku ya kipekee ambayo mashabiki watapata nafasi ya kufahamu na kukiona kikosi cha timu yao kwa ajili ya msimu mpya"
"Nawakaribisha wote waje washuhudie burudani ya aina yake kutoka kwa timu yao"

ADVERTISE HERE