Huko Ulaya majuzi klabu ya Manchester United ilitangaza kumkata mshahara wa wiki mbili mshambuliaji wake Antony Martial baada ya 'kuikacha' kambi ya klabu hiyo nchini Marekani na kurudi kwao Ufaransa kuungana na mkewe aliyejifungua.
Martial alipewa ruhusa ya siku chache hata hivyo alizidisha muda aliopewa.
Haruna Niyonzima kiungo aliyesajiliwa na Simba kutoka Yanga msimu uliopita alikosa kambi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara iliyokuwa nchini Uturuki.
Uongozi wa Simba kupitia kwa Kaimu Rais Salim Abdallah 'Try Again' umesema Niyonzima alipewa ruhusa ya kurejea kwao kushughulikia matatizo ya kifamilia, ruhusa iliyomalizika Julai 20.
Hata hivyo mchezaji huyo hakurejea nchini kwa wakati hivyo kukosa safari muhimu ya Uturuki lakini pia bado inaelezwa kuwa Niyonzima hajarudi.
Tunaamini uongozi wa Simba utamchukulia hatua stahiki kiungo huyu ili kudumisha nidhamu kwa wachezaji wote.
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko Simba.
Tabia hii ya baadhi ya wachezaji 'kujiona' haifai na inafaa ikomeshwe kwani ikiachwa iendelee itakuwa inashusha morali ya wachezaji wanaojituma kwa ajili ya timu.
Inafahamika wakati yuko Yanga Niyonzima alikuwa na kawaida ya kuchelewa kurudi kila aliporejea kwao, lakini lazima afahamu Simba ni klabu kubwa na ina taratibu zake ambazo zinafaa ziheshimiwe.

ADVERTISE HERE