Ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Simba, wanachama wa klabu bingwa Tanzania Bara, Simba wameendelea kujitolea kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba Haji Manara, leo kutakuwa na zoezi la kujitolea damu litakalofanyika Karume Ilala Boma jijini Dar es salaam.
Baadae kutakuwa na kisomo kwa ajili ya kuwaombea marehemu wote waliotangulia mbele ya hakhi.
Wakati kikosi cha Simba kikitarajiwa kuwasili leo kutoka nchini Uturuki, siku ya Jumanne wachezaji watatembelea kituo cha watoto yatima, Kawe.
Wakati huo huo klabu ya Asante Kotoko inatarajiwa kuwasili keshokutwa Jumanne, siku moja kabla ya SIMBA DAY.

ADVERTISE HERE