Aussems anaongoza benchi la ufundi kisasa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Aug 2018
Aussems anaongoza benchi la ufundi kisasa
Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua nchini Uturuki kwa ajili ya msimu ujao.

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems amefanya mabadiliko ya mfumo wa mawasiliano baina yake na uongozi.

Sasa mawasiliano yoyote ya kiofisi kuhusiana na timu kutoka kwa viongozi kwenda kwake ni lazima yawe kwa maandishi na yatumwe kwake kwa njia ya barua pepe (email) lakini pia nakala zitumwe kwa viongozi wengine wa juu yake.

Kulingana na gazeti la Championi, Aussems amekuja na utaratibu huo ili kuweka kila jambo kwenye kumbukumbu. Hata hivyo viongozi wamekuwa wakipata shida kwa kuwa bado hawajauzoea.

β€œHuo ndiyo utaratibu mpya wa mawasiliano ya ndani ya timu yetu ambao kocha amependekeza utumike, kwa hiyo na sisi hivi sasa tunajitahidi kuufanya, hivyo japokuwa unatusumbua kidogo kwa sababu tulikuwa hatujauzoea.

β€œKwa mfano tunapotoka mazoezini, daktari anatakiwa kuandika ripoti yake inayoonyesha afya za wachezaji na maendeleo ya wachezaji ambao ni majeruhi kisha amtumie kwa njia ya email huku nakala akituma kwa viongozi wengine ambao wanastahili kupata ripoti hiyo.

β€œKwa hiyo na viongozi wengine wote wanatakiwa kufanya hivyo kwa ajili ya kulinda maslahi ya timu na kuondoa hali ya kuingiliana katika kufanya maamuzi,” kilisema chanzo hicho cha habari na kukiri kuwa mfumo huo umekuwa ukiwapa wakati mgumu watendaji kwa kuwa hayakuwa mazoea yao.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo Meneja wa Simba, Richard Robart ambaye yupo na kikosi hicho nchini Uturuki hakuwa tayari kusema chochote zaidi ya kudai kuwa hayo ni mambo ya ndani ya timu kwa hiyo hawezi kuyazungumzia.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
18h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’