Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua nchini Uturuki kwa ajili ya msimu ujao.
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems amefanya mabadiliko ya mfumo wa mawasiliano baina yake na uongozi.
Sasa mawasiliano yoyote ya kiofisi kuhusiana na timu kutoka kwa viongozi kwenda kwake ni lazima yawe kwa maandishi na yatumwe kwake kwa njia ya barua pepe (email) lakini pia nakala zitumwe kwa viongozi wengine wa juu yake.
Kulingana na gazeti la Championi, Aussems amekuja na utaratibu huo ili kuweka kila jambo kwenye kumbukumbu. Hata hivyo viongozi wamekuwa wakipata shida kwa kuwa bado hawajauzoea.
βHuo ndiyo utaratibu mpya wa mawasiliano ya ndani ya timu yetu ambao kocha amependekeza utumike, kwa hiyo na sisi hivi sasa tunajitahidi kuufanya, hivyo japokuwa unatusumbua kidogo kwa sababu tulikuwa hatujauzoea.
βKwa mfano tunapotoka mazoezini, daktari anatakiwa kuandika ripoti yake inayoonyesha afya za wachezaji na maendeleo ya wachezaji ambao ni majeruhi kisha amtumie kwa njia ya email huku nakala akituma kwa viongozi wengine ambao wanastahili kupata ripoti hiyo.
βKwa hiyo na viongozi wengine wote wanatakiwa kufanya hivyo kwa ajili ya kulinda maslahi ya timu na kuondoa hali ya kuingiliana katika kufanya maamuzi,β kilisema chanzo hicho cha habari na kukiri kuwa mfumo huo umekuwa ukiwapa wakati mgumu watendaji kwa kuwa hayakuwa mazoea yao.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo Meneja wa Simba, Richard Robart ambaye yupo na kikosi hicho nchini Uturuki hakuwa tayari kusema chochote zaidi ya kudai kuwa hayo ni mambo ya ndani ya timu kwa hiyo hawezi kuyazungumzia.

ADVERTISE HERE