Waziri Mkuu mgeni rasmi SIMBA DAY

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Aug 2018
Waziri Mkuu mgeni rasmi SIMBA DAY
Mabingwa wa Soka Tanzania, Simba wamemtangaza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa ndiye atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha Simba Day.

Simba Day itakuwa Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Simba ikiivaa Asante Kotoko ya Ghana kwenye Uwanja wa Taifa.

Sherehehizo maalum za Simba hufanyika kila mwaka ambapo klabu hiyo hutumia fursa ya kutangaza kikosi chake cha msimu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema Waziri Majaliwa ndiye atakuwa mgeni rasmi huku akiwataka mashabiki wa Simba popote walipo kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

β€œWaziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ndiye atakuwa mgeni rasmi katika Simba Day tutakapocheza dhidi ya Asante Kotoko, siku hiyo ni maalum kwani itakuwa na vitu vingi ikiwemo kutambulisha wachezaji wetu wapya, hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona tukio hilo,” alisema Manara.

Manara alisema viingilio siku hiyo vitakuwa ni Sh 5000 kwa viti vya mzunguko, VIP B Sh 15,000 na VIP A Sh 20,000 ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Tundaman, Msaga Sumu, Mwasiti, Bendi ya Twanga Pepeta na nyingine nyingi

Saleh Jembe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’