Simba kurejea Jumapili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Aug 2018
Simba kurejea Jumapili
Kikosi cha Simba leo kimeendelea na mazoezi nchini Uturuki kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya Kimataifa.

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mouloudia katika mchezo wa kirafiki jana, kocha Patrick Aussems amesema anafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo huo ambao ulimalizika katika dakika ya 65 baada ya mvua kubwa kunyesha.

Simba itajifua leo, kesho na keshokutwa kabla ya kurejea nchini Jumapili, August 05 tayari kwa tamasha la SIMBA litakalofanyika August 08.

Wiki ya Simba imezinduliwa rasmi jana na itafikia tamati August 08 kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara kuchuana na Asante Kotoko katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa.

Jana Afisa Habari wa Simba Haji Manara aliwaambia wanahabari kuwa baada ya kikosi cha Simba kuwasili Jumapili, kutakuwa na zoezi la kutambulisha jezi za mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa ajili ya msimu ujao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’