Salamba awa mchezaji wa kwanza kumfungia Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Aug 2018
Salamba awa mchezaji wa kwanza kumfungia Aussems
Mshambuliaji mpya wa mabingwa wa soka Tanzania Bara Adam Salamba ameweka rekodi ya kufunga bao la kwanza la msimu wa 2018-2019 la Simba inayonolewa na kocha Mbelgiji Patrick Aussems katika sare ya 1-1 na Mouloudia Club of Oujda ya Uwanja wa Kartepe Green Park mjini Istanbul jana.

Salamba aliyesajiliwa Mei mwaka huu kutoka Lipuli ya Iringa, alifunga bao hilo kipindi cha pili baada ya kuwa sehemu ya wachezaji wote wa Simba SC walioingia kipindi hicho kuwabadili wenzao walioanza, likiwa la kusawazisha baada ya MC Oujda inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola kutangulia.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Simba SC katika kambi ya Uturuki walipowasili Julai 22 kujiandaa na msimu mpya.

Pia ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya, Mbelgiji Patrick J Aussems anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma, Mtunisia Adel Zrena Kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili na Muharami Mohammed β€˜Shilton’ kocha wa makipa na wa kwanza wa msimu pia.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’