Kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems ametumia muda wa saa mbili kufundisha wachezaji kupiga mipira ya kichwa katika mazoezi maalum yaliyofanyika jana Uturuki.
Beki wa kigeni raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa amekuwa kinara wa kupiga mipira kichwa akiwapiku wachezaji wote wa kikosi hicho.
Jana Aussems alipanga vikosi vinne na akatengeneza uwanja wenye ukubwa wa mita 30 na kutaka kila timu isimame kwenye pembe moja kabla ya wachezaji kuanza zoezi la kupiga mpira wa kichwa.
Wawa aliongoza kwa kufunga idadi kubwa ya mabao katika zoezi hilo ambapo Aussems alifurahishwa na kiwango bora cha beki huyo wa kati.
Akizungumzia zoezi hilo, kocha hiyo alisema lengo ni kuona uwezo wa kila mchezaji katika kupiga mipira ya kichwa.
βSiogopi kupiga mipira ya kichwa, mimi ni beki wa kati natakiwa niwe na uwezo mzuri katika eneo hilo,β alisema mchezaji huyo wa zamani wa Azam.
Simba imepiga kambi katika mji wa Kartepe, ikijiandaa na mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza mwezi ujao pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE