Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, kesho Jumatano, August 01 2018 kitashuka dimbani nchini Uturuki kuikabili Moulodia kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa jiji la Istanbul saa kumi kamili jioni.
Simba imeweka kambi ikijifua nchini Uturuki kwa takribani wiki moja sasa.
Mchezo huo wa kesho utatoa nafasi kwa benchi la ufundi kufahamu ni kwa kiasi gani wamefanikiwa na kambi hiyo.
Pia mchezo huo utatoa nafasi kwa benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu Patrick Aussems kufahamu uwezo wa wachezaji wake nje ya mazoezi.
Huo ndio mchezo wa kwanza wa kirafiki wa Simba tangu itue nchini Uturuki wiki iliyopita.

ADVERTISE HERE