Wakati kesho ikitarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mouloudia, uongozi wa Simba umesema utaweka hadharani hivi karibuni timu alikwa kwenye tamasha la SIMBA DAY litakalofanyika August 08.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema sasaa ni mapema sana kuitaja timu watakayocheza nayo kwani bado nguvu zao zipo katika maandalizi ya msimu ujao ambapo timu imeweka kambi Uturuki.
Manara amesema kuelekea tarehe 2 mpaka 3 Agosti timu hiyo itawekwa wazi lakini kwa sasa haiwezi kutajwa akieleza kuwa wakati mwafaka haujawadia.
Kikosi cha Simba kinaendelea kujifua nchini Uturuki yakiwa ni maandalizi ya msimu mpya na mcihuano ya Kimataifa.

ADVERTISE HERE