Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kiungo Haruna Niyonzima ambaye bado hajaungana na wenzie Uturuki, atarejea nchini kesho akitokea kwao Rwanda.
Manara amesema Niyonzima alipewa ruhusa na uongozi wa Simba akidai kuwa na matatizo ya kifamilia. Anatarajiwa kurejea kesho.
Huenda mchezaji huyo asiungane na wenzie nchini Uturuki kwani Simba inatarajiwa kurejea August 05, siku tatu kabla ya SIMBA DAY.
Tayari amekosa mazoezi kwa takribani wiki nzima na kwa siku zilizosalia hakuna uwezekano wa yeye kusafiri.
Awali mchezaji huyo alishindwa kusafiri na wenzake kutokana na pasi yake ya kusafiria kuwa na matatizo.
Niyonzima ndiye mchezaji pekee wa kikosi cha kwanza cha Simba ambaye hayuko kambini nchini Uturuki.

ADVERTISE HERE