Niyonzima bado kutua Uturuki kulikoni?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
28 Jul 2018
Niyonzima bado kutua Uturuki kulikoni?
Kiungo mchezeshaji wa Simba Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ni kama ameikacha kambi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara baada ya viongozi kulalamika kutopokea simu kila wakimtafuta hewani.

Kiungo huyo alitakiwa kuwepo kwenye msafara wa wachezaji wanne waliosafiri juzi kuelekea Uturuki kujiunga na wenzao lakini hakuwepo huku wenzake, Said Ndemla, Hassani Dilunga, Meddie Kagere na Erasto Nyoni wakiwa wametua na kuanza kujifua.

Mnyarwanda huyo alijiunga na Simba kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika wa miaka miwili.

Inadaiwa Niyonzima bado yupo nyumbani kwao Rwanda alipokwenda kwenye mapumziko.

Niyonzima alitakiwa kuripoti Dar wiki moja iliyopita kabla ya timu kuelekea Uturuki, lakini alikaidi agizo alilopewa na uongozi na sababu ni kibali chake cha kuisafiria ‘paspoti’ kumalizika.

“Awali, Niyonzima alituambia kuwa paspoti yake imemalizika tukamuambia atutumie kwa ajili ya kumtengezea mpya akatutumia, lakini tangu alipotutumia ikawa kimya.

“Tumejaribu kumtafuta mara kwa njia ya simu kwa kumpigia wakati mwingine simu inaiita lakini haipokelewi, tukimtafuta wakati mwingine simu yenyewe haipatikani, hivyo tunashindwa kumuelewa.

“Inavyoonekana kama hataki kujiunga na kambi ya Uturuki, hivyo kama uongozi tumeona tuachane naye atakapojisikia kujiunga na timu atakuja kwa sababu yeye anafahamu kabisa timu ipo kwenye ‘pre season’ alitakiwa kuwa na timu pamoja,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Niyonzima kuzungumzia hilo simu yake mkononi ilikuwa haipatikani na alipotafutwa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa ‘WhatsAp’ meseji yake haikufika kujibu hilo.

Championi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →