Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji amesema malengo makuu ya klabu hiyo ni kuwa miongoni mwa vilabu bora 10 barani Afrika.
Tangu ashinde zabuni na kumiliki hisa kwa asilimia 49, Mo amedhamiria kufanya mabadiliko makubwa Simba ili aweze kutimiza ndoto hiyo.
Baada ya uwekezaji uliofanyika msimu uliopita kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kusubiri kwa misimu mitano, msimu huu Simba imedhamiria kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa pia.
Mo amefanikisha ujio kocha Patrick Aussums aliyechukua nafasi ya Pierre Lechantre lakini pia Simba imefanya usajili makini.
Malengo makuu ya klabu ya Simba msimu huu ni kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Simba iko nchini Ituruki ikiendelea na maandalizi kwa ajili ya michuano ya msimu unaoanza mwezi ujao.

ADVERTISE HERE