Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya Simba Haji Manara ameishukia Clouds FC redio kwa kutangaza taarifa za uongo zinazoihusu Simba.
Mapema leo redio hiyo ilitangaza kuwa Simba imecheza mchezo wa kirafiki nchini Uturuki na kufungwa mabao 6-0 jambo ambalo halina ukweli wowote.
Manara ameitaka redio hiyo ithibitishe ukweli wa taarifa yao au ikanushe na kuomba radhi.
"Ndugu zangu wa Clouds with do respect mnachotufanyia si haki na mnatukosea sana tena sana," amesema Manara
"Leo mmetangaza kwenye Radio yenu Simba imecheza mechi Uturuki na kufungwa 6-0.
"Tunaomba mthibitishe au mkanushe. Vinginevyo mtakuwa na nia ovu ya kutudhalilisha na kwa hili hatutawaelewa na hatutakubali!
"Mimi wajibu wangu pia ni kulinda image ya Club yangu na sipo tayari kuona Chombo chochote kikitangaza taarifa ya uzushi na uongo dhidi ya Simba kwa kisingizio chochote kile.
"kwa hili nategemea mtachukua hatua stahiki haraka iwezekanavyo vinginevyo thibitisheni

ADVERTISE HERE