Kagere, Nyoni, Niyonzima kutua Uturuki kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jul 2018
Kagere, Nyoni, Niyonzima kutua Uturuki kesho
Wakati kikosi cha Simba kikiendela kujifua kwenye kambi maalum ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, wachezaji wengine wanatarajiwa kukwea pipa kesho Jumatano.

Wachezaji hao ni Meddie Kagere aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC, Haruna Niyonzima na Erasto Nyoni ambao viza zao za kusafiria zilichelewa kukamilika.

Kuchelewa kwa viza zao kulisababisha washindwe kwenda na kikosi kilichosafiri Jumapili hivyo ikabidi wasalie nchini mpaka pale taratibu nzima za kuzikamilisha zitakapomalizika.

Kikosi hicho kipo Instabul kikijifua kwa maandalizi ya tamasha la Simba litakalofanyika Uwanja wa taifa, Dar Es Salaam, Agosti 8 2018 kama ilivyo ada.

Simba hufanya tamasha hilo maalum kuwatambulisha wachezaji wao watakaokuwepo kwenye kikosi cha msimu wa 2018/19.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’