Mshambuliaji mpya wa Simba Meddie Kagere hakuwa katika kundi la wachezaji waliosafiri leo kwenda nchini Uturuki sababu ikielezwa kuchelewa kwa VISA yake.
Kulingana na mmoja wa viongozi wa Simba, Kagere alikwenda kwao kushughulikia matatizo ya kifamilia na aliporejea alikuta mchakato wa kuwakatia VISA wachezaji umeshafanyika.
Mshambuliaji huyo atasafiri mara moja baada ya kupata VISA.
Mbali na Kagere, wachezaji wengine walioshindwa kuondoka leo ni pamoja na Haruna Niyonzima, Mwinyi Kazimoto, Adam Salamba na Erasto Nyoni.
Nyoni alipewa ruhusa ya kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia wakati Niyonzima Passport yake ina matatizo.
Salamba anaendelea na matibabu ya majeraha aliyoumia kwenye michuano ya kombe la Kagame, huku Mwinyi Kazimoto akidaiwa kutimkia JKT Tanzania.
Wachezaji hao wanatarajiwa kusafiri kuungana na wenzao baada ya michakato yao kukamilika

ADVERTISE HERE