Mo Rashidi 'apagawa' na maisha ya Msimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jul 2018
Mo Rashidi 'apagawa' na maisha ya Msimbazi
Mshambuliaji mpya wa Simba, Mohamed Rashid amekiri kwamba maandalizi yao kuelekea msimu mpya wa 2018/19 ni makubwa tofauti na alikotoka Prisons.

Mo Rashid amesema namna ambavyo matajiri wa timu hiyo wanavyopanga mikakati ya namna watakavyotetea ubingwa na kumtaka kila mchezaji atambue wajibu wake na kujua kwa nini yupo kwenye timu.

"Naendelea kujifunza vitu vingi vinavyonibadilisha mtazamo, kuona naweza nikafika mbali zaidi, kikubwa natakiwa kujituma na kujitunza mwili wangu kuwa tayari kwa ajili ya majukumu.

"Nimeamini kweli Simba ni klabu kubwa, unajua hata inakuamsha mchezaji kuwaza vitu vikubwa kutokana na jinsi ambavyo mabosi wanavyotazama mbali na kuwa na malengo makubwa," alisema Rashid.

Mohamed anasema anaamini msimu ujao kwake utakuwa na manufaa yatakayotokana na ushindani wa kuwania namba mbele ya wakongwe wanaoamini ndani ya kikosi hicho.

"Ushindani unamfanya mchezaji kuwa bora kwani kila wakati anakuwa anaboresha kiwango chake akiogopa kupiga benchi, unajua tofauti na pale unapoona wewe ndiye tegemeo la kwanza," alisema Mo Rashid.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’