Omog aikamia Stand United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Sep 2017
Omog aikamia Stand United
Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog amesema kikosi chake kimejipanga kuondoka na ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Stand United Jumapili ijayo.

Omog amesema baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC jijini Mwanza, amefanyia marekebisho mapungufu yaliyopelekea timu yake ikose ushindi kwenye mchezo huo licha ya kucheza vizuri.

"Naweza kusema hiyo ni sawa na vita kwani ushindi ndiyo jambo la msingi kwasasa ukizungatia wenzetu wakubwa nao wanashinda kwenye mechi zao hivyo nasisi tulazimika kushinda ili kujiweka sehemu salama," amesema Omog.

Simba iko jijini Mwanza ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa Jumapili, Oktoba 01.

Kocha huyo amesema pia kiungo wake Shiza Kichuya, aliyeumia na kutoka dakika ya 44, kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC, anaendelea vizuri na hadi kufikia siku ya mchezo atakuwa fiti kwa ajili ya kuichezea timu yake.

Kocha huyo amesema bado mapambano yao yanaendelea kuhakikisha wanashinda kila mechi na kutwaa taji hilo ambalo sasa imepita misimu minne bila kulitwaa.

Simba na Yanga zinalingana kwa pointi hivisasa zote zikuwa na pointi nane lakini Simba wanaongoza kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’