Msafara wa watu 35 wa kikosi cha Simba ukijumuisha viongozi, wachezaji na benchi la ufundi umeondoka kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.
Msafara huo uligawanywa kwenye makundi mawili ambapo kundi la kwanza liliondoka jana likiongozwa na Kocha Msaidizi, Masoud Djuma pamoja na Kocha wa Makipa, Mohamed Mwarami, Daktari wa timu, Yassin Gembe na meneja wa timu hiyo.
Kundi la pili lililojumisha wachezaji limeondoka Alfajiri ya leo.

Simba itafikia na kuweka kambi kwenye mji maarufu wa Antalya.
Mapema jana, kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma alisema wiki mbili watakazokuwa kwenye mji huo wenye viwanja vingi vya kisasa wamepanga kucheza mechi tatu za kirafiki ambapo wiki ya kwanza baada ya kufika watafanya mazoezi na ile ya pili ndiyo watajipima.
"Hatutacheza mechi nyingi ni mbili au tatu inategemea na siku ambazo tutakaa," alisema.

ADVERTISE HERE