Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wamemtambulisha Patrick Aussems kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo.
Aussems amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Simba mbele ya Kaimu Rais Simba Salim Abdallah (Try again) pamoja na Kaimu Makamu Rais Idd Kajuna.
Utambulisho wa kocha huyo Mbelgiji anayechukua nafasi ya Pierre Lechantre umefanywa mapema leo Alhamisi kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkuu wa idara ya Habari ya klabu ya Simba Haji Manara amesema kocha huyo ana uzoefu wa soka la Afrika na ameteuliwa baada ya jopo la wataalam waliomfanyia usaili kujiridhisha na uwezo wake.
Kocha huyo amewahi kuzinoa timu kadhaa za Afrika ikiwemo AC Leopards ya Congo, KSA Cameroon ya Cameroon na ES Troyes AC ya Ufaransa
Makocha 57 waliomba nafasi ya ukufunzi wa Simba, Aussems amewazidi sifa makocha wengine wote walioomba kazi hiyo.
Manara amesema lengo la Simba kumteua kocha huyo ni kuhakikisha Simba inatetea ubingwa wake iliyotwaa msimu uliopita lakini pia kufika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

ADVERTISE HERE