Kambi ya kikosi cha Simba kujiandaa na msimu mpya pamoja na michuano ya Kimataifa sasa itakuwa nchini Uturuki ambapo imeelezwa kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara huenda wakakwea pipa kesho Ijumaa.
Kambi hiyo ya siku 15 itahitimishwa August 05 siku tatu kabla ya SIMBA DAY.
Simba inakwenda Uturuki ikiwa na kikosi chake kamili kitakachojumuisha wachezaji waliopewa mapumziko wakati wa michuano ya kombe la Kagame.
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma amesema kambi hiyo itawasaidia kutengeneza kikosi imara.
Amesema ameridhishwa na viwango vilivyoonyeshwa na baadhi ya wachezaji kwenye michuano ya kombe la Kagame na anaamini sasa wote wanaanza upya kusaka kikosi cha kwanza.
Usajili wa baadhi ya wachezaji wapya utaongeza ushindani wa namba kwenye kikosi cha Simba ambapo Djuma amesisitiza wachezaji watakaopata nafasi ni wale watakaokuwa na viwango bora na si kuangalia majina.
Kocha Mpya wa Simba Patrick Aussems raia wa Ubelgiji anatarajiwa kuungana na kikosi hicho nchini Uturuki.

ADVERTISE HERE