Julio atia neno ongezeko la 'maproo' 10

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jul 2018
Julio atia neno ongezeko la 'maproo' 10
Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameshangwa na uamuzi uliotolewa hivi karibu na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuruhusu klabu kusajili wachezaji 10 wa kigeni na wanaruhusiwa kuwatumia wote wa wakati mmoja akitamka kuwa hatma ya Taifa ni mbaya.

Rais wa TFF, Wallece Karia alitangaza ongezeko hilo kutoka wachezaji saba hadi 10 kuanzia msimu ujao ambapo zinaruhusiwa kusajili katika usajili huu unaoendelea.

Julio alisema licha ya uwepo wa wachezaji wengi wa kigeni ambao wataongeza changamoto kwa wazawa lakini haungi mkono ongezeko hilo ili kunusuru viwango vya wachezaji wa ndani ambao ndio wanawajibika kutumikia timu za Taifa.

Ò€œSawa kanuni mpya ya kuongezeka kwa wachezaji wa kigeni inaweza kuwa na maana kwa jinsi walivyoipitisha walivyohisi na pia itaongeza changamoto kwa wachezaji wazawa lakini bado sijaunga mkono uamuzi huo kwa sababu utaathiri soka letu na hata timu zetu za taifa,Ò€ alisema Julio

Julio aliongeza kuwa wachezaji wazawa wanapaswa kuwa sehemu ya lawama hizi za kusababisha wachezaji wa kigeni kuongezeka kwa sababu wachezaji wengi wanashindwa kutambua wajibu wao kuhakikisha wanajituma ipasavyo ili timu zao zisihangaike kutafuta wachezaji wa nje.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’