Manara afunga mjadala wa Yondani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jul 2018
Manara afunga mjadala wa Yondani
Baada ya kuweko kwa taarifa kuwa Simba ilikuwa mbioni kumsajili beki mkongwe kutoka Yanga, Kelvin Yondani, Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema mpango huo haupo.

Manara amesema taarifa hizo zimetengenezwa makusudi ili kuwafariji mashabiki wa Yanga siku timu hiyo ikitangaza imemsainisha mkataba mpya.

"Ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe, wameamua kuvujisha taarifa hizo makusudi wasake pesa kisha wakija kumsajili waseme wameipiga bao Simba. Sisi hatumuhitaji wala hatuna mpango naye" amesema Manara.

Wakati huo huo kikosi cha Simba kimeendelea kujifua kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam kujiandaa na msimu mpya wa VPL pamoja na michuano ya Kimataifa.

Simba inatarajiwa kwenda nchini Uturuki wakati wowote kuweka kambi ya siku 18 kabla ya kurejea kwa ajili ya Simba Day, August 08 2018.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’