Manara afafanua Mkutano wake na Wanahabari

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Nov 2017
Manara afafanua Mkutano wake na Wanahabari
Kiasili Haji Manara sio mtu dhaifu anayeweza kukalia kimya shutuma zinazokuja kwake binafsi au taasisi anayoingoza na kuifanyia kazi, ni aina ya mtu anayejua thamani ya habari, anaetaka na kuamini usahihi wa jambo liliopo na linalokuja kwa kadri lilivyo.

Nimeanza na dokezo hilo kusudi ili tuende sawa kwanza, ili kujibu tuhuma na shutuma zinazoelekezwa na baadhi ya magwiji wa ukosoaji nchini hususan kwenye tasnia yetu hii ya kandanda nchini.

Baada ya mkutano wangu na vyombo vya habari hapo jana jnne ya tarehe 31-10-2017 pale klabuni Msimbazi, kumetokea wakosoaji wakubwa dhidi yangu binafsi, na wengine wakienda mbali zaid kwa kunifananisha hata na msemaji wa klabu ya Yanga.

Nianze na hili la maudhui ya mkutano wangu wa jana na wanahabari.

kwanza niweke wazi kama mtu nnayesimamia idara ya Habari ya klabu, sina mamlaka yoyote ya kuitisha press bila idhini ya uongozi wa klabu ya Simba, na ktk hili simjui yoyote afanyae kazi kama yangu mwenye mamlaka ya kuongea na waandishi bila idhini ya Uongozi wa taasisi anayoifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, press yangu ya jana ina baraka zote za uongozi wa Simba SC, na maudhui ya nilichokizungumza jana ni matakwa halali ya uongozi.

Lakini pia niuarifu umma kuwa bado ninaamini pamoja na wanadaam kutokuwa wakamilifu, waamuzi waliochezesha mchezo wa jmosi dhidi ya Yanga na wale waliochezesha michezo mingine niliyoizungumzia jana, kuna makosa waliyafanya na mm kama msemaji wa klabu, ilikuwa ni wajibu wangu kuzungumzia hilo.

Inawezekana labda kwa baadhi ya watu haikuwa sahihi kwao, lakini dhamira ya klabu ya Simba sio kushutumu, bali ni kutaka 'fair game' hatutaki kupendelewa wala kuonewa, na ndio maana nilitoa TV Set ofisini kwangu na kuileta kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu, ili kile nnachokiongea kipate legitimacy na sio kuleta porojo za mtaani.

Bahati mbaya sana wale wakosoaji badala ya kujikita na hoja zangu, wakaamua kunishambulia binafsi, na hata walipoamua kujibu hoja waliegemea kishabiki zaidi, huku wakiangalia dhamira za wachezaji bila kuangalia uhalisia wa kisheria na matakwa ya pigo la penati linatolewa.

HAJI S. MANARA
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’