Manara akanusha Simba kumsajili Yondani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jul 2018
Manara akanusha Simba kumsajili Yondani
Kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mabingwa wa Tanzania Bara, Simba wanakaribia kumalizana na beki wa Yanga Kelvin Yondani.

Yondani anadaiwa kugoma kusaini mkataba mpya na klabu ya Yanga swala la 'ukata' wa klabu hiyo ikielezwa kuwa sababu ya beki huyo mkongwe kutaka kutimka.

Lakini Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba Haji Manara amesema mpaka sasa hana taarifa rasmi ya klabu kuhusu ukweli wa taarifa hiyo.

"Shida yangu mm ni moja tu, jambo linazushwa halafu napigiwa eti nithibitishe! Kawaulizeni waliotoa taarifa hii. Simba haipo, na mimi ndio spokesman wa klabu," ameandika Manara kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Kumekuwa na mjadala miongoni mwa mashabiki wa Simba ambapo wengi wao wamependekeza beki huyo aliyemaliza mkataba na klabu ya Yanga asajiliwe ili kuongeza nguvu zaidi kwenye safu ya ulinzi.

Hata hivyo matukio yake ya utovu wa nidhamu hasa tukio la kumtemea mate beki Asante Kwasi kwenye mchezo wa watani wa jadi msimu uliopita yamewakasirisha wengi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’