Simba yamrejesha Kakule Rwanda, ni baada ya Kiyovu kumuwekea ngumu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
17 Jul 2018
Simba yamrejesha Kakule Rwanda, ni baada ya Kiyovu kumuwekea ngumu
Kiungo Mkongomani Kakule Fabrice aliyekuwa akifanya majaribio katika timu ya Simba ameondoka nchini na kurudi kwao ili kwenda kumalizana na mabosi wake wa Kiyovu.

Fabrice aliyetua nchini wiki mbili zilizopita ili kufanya majaribio na kama akifanya vizuri ajiunge na timu, lakini mabosi wa Simba wameshtukia kusikia kumbe ana mkataba na klabu yake ya zamani na hakuondoka vema huko kwao.

Kiungo huyo aliyewahi kufundishwa na Kocha wa Simba, Masoud Djuma wakati akiwa Rayon Sports aliondoka usiku wa juzi Jumamosi ili kwenda kuweka mambo sawa na kama utamkubalia na mabosi wake arudi na barua la sivyo ndio basi.

“Unajua Fabrice alipendekezwa na kocha Djuma akitaka asaini moja kwa moja, ila tuliomba afanye mazoezi ili amuangalie vizuri maana kama kumfundisha ilikuwa siku nyingi kipindi wapo Rayon,” mmoja wa vigogo wa usajili wa Simba alisema.

“Tukiwa tunamuangalia ndipo zikaja taarifa kwamba hakuondoka vema kwao, kwani bado ana mkataba wa miaka miwili na tusingemsajili mpaka akamalizane na uongozi wake ili kuepuka shida kutoka CAF au FIFA,” alisema.

Hata hivyo, kuondoka kwa Fabrice huenda ndio ikawa kimoja kwani tayari Simba imemsainisha kiungo toka Mtibwa Sugar, Hassani Dilunga huku ikiwa na vifaa vingine katika nafasi hiyo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →