Mshambuliaji mpya wa Simba Adam Salamba amethibitisha kuwa ni kweli jana alipata ajali ya gari alipokuwa akitokea kwao mkoani Mwanza.
Ajali hiyo imetokea eneo la Vigwaza, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Salamba amesema ajali hiyo ilihusisha magari matatu ambapo gari yake iligongwa na gari nyingine nyuma kupelekea naye kugonga gari iliyokuwa mbele yake.
Yeye pamoja na abiria wengine wawili waliokuwa kwenye gari yake hawakupata majeraha yoyote.
Γ’β¬ΕNilikuwa natoka Mwanza kuja Dar, nilipofika Vigwaza kulikuwa kuna foleni, nikasimama mara kama dakika mbili nasikia nyuma kishindo gari imegongwa, ikasukumwa mbele ikangonga gari nyingine, cha kushukuru sijaumia, niko salama.Γ’β¬Β

ADVERTISE HERE