Shughuli imekwisha Urusi, Ufaransa bingwa wa dunia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jul 2018
Shughuli imekwisha Urusi, Ufaransa bingwa wa dunia
Ufaransa imefanikiwa kutwaa kombe la dunia kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka 20 baada ya kuilaza Croatia mabao 4-2 kwenye mchezo wa fainali.

Ufaransa imerudia kile ilichofanya mwaka 1998 wakati michuano hiyo ilipofanyika katika ardhi yao ya nyumbani.

Licha ya kuanza taratibu mchezo huo, Ufaransa ilikwenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 2-1 ikitumia nafasi mbili za adhabu kufunga mabao yake kupitia Antoine Griezmann aliyefunga bao la pili kwa mkwaju wa penati huku bao la kwanza likiwa la kujifunga, Mario Mandzukic.

Bao la Croatia lilifungwa na Ivan Prisic.

Kipindi cha pili Ufaransa ilijihakikishia ubingwa baada ya kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Kylian Mbappe na Paul Pogba.





Bao la pili la Croatia lilifungwa na Mandzukic aliyefuta makosa yake ya kujifunga baada ya kutumia vyema uzembe wa mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris.

Klyan Mbappe ameibuka kuwa mchezaji bora chipukizi wa michuano hiyo ambayo amefunga mabao manne.





Amekuwa mchezaji wa pili mdogo kufunga bao kwenye mchezo wa fainali baada ya Pele.



Harry Kane wa Uingereza ameibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao sita wakati kipa bora wa mashindano hayo amekuwa Thibaut Courtois wa Ubelgiji.

Luka Modric ndiye mchezaji bora wa michuano hiyo.



Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps ameingia kwenye rekodi ya kushinda taji hilo akiwa mchezaji mwaka 1998 na mwaka huu akiwa kocha.

Wengine waliowahi kufanya hivyo ni Mario Zagalo wa Brazil na Franz Beckenbauer wa Ujerumani.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’