Kagere anawasubiri kwa hamu Bocco, Okwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
15 Jul 2018
Kagere anawasubiri kwa hamu Bocco, Okwi
Straika aliyeng'ara na Simba kwenye Kagame, Meddie Kagere amesema kwamba endapo wachezaji walioko likizo wakirejea kwenye timu hiyo akiwemo Emmanuel Okwi na John Bocco kikosi hicho kitatisha sana.

Kagere ametua Simba hivi karibuni akitokea Gor Mahia ya Kenya ambayo mashabiki wao mpaka leo hawaamini kilichotokea mpaka akawakimbia. Amefunga mabao manne kwenye Kagame.

Raia huyo wa Rwanda ambaye jana Jumamosi aliondoka kwenda kwao kukamilisha mambo yake amesema; “Unajua asilimia kubwa ya wachezaji wengi ambao tulikuwa tunacheza ndiyo mara yetu ya kwanza kuwa hapa sasa imechangia kwa namna fulani hivi kushindwa kupata kile ambacho tunakitaka kwenye Kagame.”

“Ninaamini kwamba wakija wachezaji wengine walio mapumziko (Okwi na Bocco) na kupata muda mzuri wa kujiandaa basi nikwambie tu hakuna ambaye atakuwa na uwezo wa kutuzuia sisi kwa msimu ujao, niwaambie tu mashabiki wasubiri,” alisema Kagere ambaye amezaliwa Uganda.

Kocha wa Simba, Masoud Djuma aliwapa mapumziko wachezaji waliotumika kwa asilimia kubwa kwenye ligi wakiwemo Okwi, Bocco, Aishi Manula, Haruna Niyonzima, Jonas Mkude na wengineo.

Championi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →