Omog azitumia salamu Prisons, Mbeya City

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
1 Nov 2017
Omog azitumia salamu Prisons, Mbeya City
Baada ya matokeo ya sare dhidi ya Yanga kikosi cha Simba kinaelekea mkoani Mbeya ambako kitacheza michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Prisons Novemba 05 na Novemba 18.

Kuelekea michezo hiyo, kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameweka wazi kuwa anataka kuvunja rekodi ambayo ni kuibuka na pointi sita.

Omog na jeshi lake la Simba litakuwa na kibarua kigumu cha kucheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mara kwa mara wamekuwa na matokeo mabaya, ambapo Jumapili watawavaa Mbeya City kwenye uwanja huo kisha kumaliza na Prisons, Novemba 18, mwaka huu.

Mcameroon huyo amesema pamoja na rekodi mbaya kila wanapocheza uwanjani hapo lakini safari hii hawataruhusu hilo litokee kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa pointi tatu za kila mchezo.

“Tunajua kuwa mara kwa mara tunasumbuka kupata matokeo hapa Sokoine, lakini safari hii sitakubali kuona hilo linatokea tayari tumeshaweka mikakati kabambe ya kupata pointi sita kutoka kwa wenyeji wetu.

“Tunataka tushinde kwa ajili ya kujiongezea wigo wa pointi dhidi ya mahasimu wetu ambao tunalingana nao kwenye msimamo, na hatuwezi kuwakimbia bila ya kupata matokeo mazuri hasa kwenye mechi kama hizi za ugenini.

“Niseme wazi kwamba lile suala eti la kuwa na rekodi ya kupoteza mechi kila tunapokuwa hapa Mbeya kwa sasa ndiyo limefika mwisho,” alisema kocha huyo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →