Kinara wa mabao Medie Kagere, amesema atajisikia fahari kama watatwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame.
Kagere amesajiliwa na Simba mwishoni mwa mwezi Juni, akianza kuitumikia timu hiyo kwenye michuano ya Kagame. Tayari ameifungia Simba mabao matatu kwenye michuano hiyo.
Kagere amefurahia kuwa na mchango katika kikosi cha Simba kwenye michuano hiyo ya Kagame.
"Ni kazi ya timu nzima na si mimi peke yangu, nafurahi kuona tunacheza fainali, nitafurahi kuchukua ubingwa nikiwa bado mgeni hapa," amesema Kagere.
Kagere amesema amefuhari kuona Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa na wanampa ushirikiano unaomrahisishia kazi yake uwanjani.
Mkali huyo wa mabao raia wa Rwanda ambaye alizaliwa na kukulia nchini Uganda leo atakiongoza kikosi cha Simba kwenye mchezo wa fainali kombe la Kagame dhidi ya Azam FC.
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 12 jioni kwenye uwanja wa Taifa.

ADVERTISE HERE