Simba yaiwinda Azam FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Jul 2018
Simba yaiwinda Azam FC
Kikosi cha Simba leo jioni kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa fainali kombe la Kagame dhidi ya Azam FC utakaopigwa leo Ijumaa, Julai 13 kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12 jioni baada kukamilika kwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Gor Mahia dhidi ya JKU utakaopigwa saa tisa Alasiri.



Kaimu kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma amesema wamejiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Simba huenda ikaendelea kumkosa mshambuliaji wake Adam Salamba aliyechanika nyama za paja kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya AS Ports.

Hata hivyo wachezaji wengine wote wakiongozwa na kinara wa mabao Meddie Kagere wako katika hali nzuri, tayari kuibeba Simba kwenye mchezo huo.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa ni mchezo wa fainali utakaohusisha timu zinazofahamiana lakini ana imani kubwa kwa Simba kuibuka na ushindi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’