Yanayojiri Urusi : Dharau zawaponza Waingereza

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Dharau zawaponza Waingereza
Kipigo cha mabao 2-1 ilichopata Uingereza kutoka kwa Croatia kimewanyong'onyeza mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wameanza kuamini kombe la dunia linaelekea Uingereza.

Shamrashamra zilianza mapema Uingereza baada ya timu hiyo kutinga nusu fainali lakini bao la Mario Mandzukic kwenye muda wa zaidi lilizima shamrashamra hizo.

Kwenye mchezo huo wa nusu fainali, Uingereza ilitangulia kufunga bao la kuongoza mapema tu kwenye dakika ya tano mfungaji akiwa Kylian Trippier kupitia mpira wa adhabu.

Hata hivyo ni Croatia iliyotawala mchezo huo kwa kutengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha pili na ilifanikiwa kusawazisha bao kwenye dakika ya 68 mfungaji akiwa Perisic.

Baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 na Uingereza ikapoteza mchezo huo kwenye muda wa nyongeza.

Hii ni mara ya pili kwa Uingereza kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali. Iliondolewa katika hatua hiyo mwaka 1990

Croatia imeandika historia mpya ya kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Nchi hiyo ina wananchi milioni nne tu.

Baada ya ushindi huo nahodha wa Croatia Luka Modric amewapiga kijembe waingereza kuwa waliingia uwanjani wakiwa na matokeo mfukoni.

Aidha amevikosoa vyombo vya habari vya Uingereza kwa kuidharau Croatia.

Croatia itacheza na Ufaransa kwenye mchezo wa fainali Jumapili Julai 15, wakati Uingereza itachuana na Ubelgiji kusaka mshindi wa tatu Julai 14.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’