Julio awataka wachezaji wa Simba wabadilike

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Oct 2017
Julio awataka wachezaji wa Simba wabadilike
Kocha wa zamani na mdau mkubwa wa klabu ya Simba Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameipongeza Yanga kutokana na kiwango bora, ambacho imekionyesha kwenye pambano la Jumamosi na kupata sare ya kufunga bao 1-1.

Julio amesema kwa namna alivyouangalia mchezo ule Yanga, ndiyo timu iliyostaili ushindi, kutokana na kuonyesha soka safi na mashambulizi mengi kwenye lango la Simba lakini walikosa bahati ya kufunga na umahiri wa kipa Aishi Manula, ulisaidia kuwaokoa.

"Mimi ni mwanachama mkubwa wa Simba, lakini kusema ukweli Yanga walituzidi sana na walistaili kupata ushindi kwasababu walicheza kwa ushirikiano na kujituma lakini walichokikosi ni bahati ya kutumbukiza mpira wavuni," amesema Julio.

Kocha huyo ambaye kwasasa anakinoa kikosi cha Dodoma FC, kwenye daraja la kwanza, amesema kilichoiponza Simba, katika mchezo huo ni wachezaji kushindwa kutekeleza majukumu yao huku kila mmoja akijiona yeye ndiyo bora zaidi ya mwenzake.

Amesema pamoja na kusajili majina makubwa lakini bado wachezaji wanapaswa kuacha matabaka na kuweka juhudi kwenye kuipigania timu ili waweze kufikia malengo ambayo ameyakusudia msimu huu.

Julio amesema kama Simba, wataendelea kucheza hivyo kwenye mechi zinazokuja, itakuwa vigumu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu huu kwani Yanga bado wameonyesha ni timu bora na itaendelea kuwa fiti zaidi siku zijazo kwasababu baadhi ya wachezaji wake mahiri waliokuwa majeruhi kwasasa watapona na kurudi uwanjani.

Mbali na Julio, mkongwe mwingine wa Simba Boniface Pawasa nae amehoji ari ya wachezaji katika mchezo huo ambao wachezaji wa Simba walifanya makosa mengi yaliyowapa nafasi Yanga kupeleka mashambulizi ya hatari langoni hivyo kumpa kazi ya ziada mlinda lango namba moja nchini Tanzania, Aishi Manula.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’